KCSE Revision AI kcserevision.app

KCSE 2024 Kiswahili Paper 3

The KCSE 2024 Kiswahili Paper 3 (102/3). Fasihi: riwaya, tamthilia, hadithi fupi, ushairi na fasihi simulizi. View it below, download it to print, or revise it with the AI tutor, which takes you through each question and marks your answers. Source: Teacher.co.ke.

102/3 · KISWAHILI · Karatasi 3 (Fasihi) · Nov. 2024 · Saa 2½

Maagizo: Jibu maswali manne pekee. Swali la kwanza ni la lazima. Maswali mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani Riwaya, Tamthilia, Ushairi na Fasihi Simulizi. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.

Sehemu A: Hadithi Fupi

D.W. Lutomia na P. Muthama (wah.): Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine

1. (Lazima)
(a) D. Ogutu: "Toba ya Kalia"

"…alikuwa na kibarua kigumu. Angesema nini? Hata hivyo, lisilobudi hubidi. Maji alikwishayavulia nguo, sharti ayaoge."

 (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 (ii) Fafanua umuhimu wa mhusika anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)
(b) Fafanua jinsi mbinu ya majazi imetumika katika kujenga vipengele vifuatavyo katika hadithi ya "Pupa": (i) wahusika (alama 5); (ii) maudhui (alama 5).

Sehemu B: Riwaya

C. Momanyi: Nguu za Jadi — Jibu swali la 2 au la 3.

2. (a) "Tulia mheshimiwa. Mambo yatakuwa sawa. Ni mapema mno kujua kinachoendelea."
 (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 (ii) Bainisha toni katika dondoo hili. (alama 2)
 (iii) Fafanua sifa sita za anayezungumza kwa kurejelea riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 6)
(b) "Ulevi una athari kwa jamii." Thibitisha kwa kurejelea riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 8)

3. (a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo: (alama 8)

"Nyuso zilizoghadhibika zilidhihirisha furaha, angalau kwa muda tu. Waketwa ni watu waliokuwa na maarifa ya ujasiriamali tangu zamani. Hakuna aliyejua kwamba eneo la Matango lingezalisha kitu. Lilikuwa kichaka kikavu kilichohamwa hata na panya. Leo limekuwa eneo la maendeleo ya kupigiwa mfano. Si majumba makubwa ya aushi, si ghorofa na wingi wa maduka. Hata watu waishio katika mitaa ya kifahari, walikuja kununua bidhaa hapo. Kulikuwa na bidhaa mbalimbali zilizouzwa kwa bei ya rejareja au ya jumla. Kando kidogo na sehemu hii ya biashara, watu walijenga nyumba za kuishi. Hapa ndipo palipokuwa pakiishi idadi kubwa ya Waketwa. Sasa wamechomewa makazi yao na kufurushwa. Wamekuwa kama wahamiaji wasiotakikana kuishi nchini Matuo."

(b) "Suala la dhuluma dhidi ya mwanamume limeshughulikiwa katika riwaya ya Nguu za Jadi." Thibitisha. (alama 12)

Sehemu C: Tamthilia

T.M. Arege: Bembea ya Maisha — Jibu swali la 4 au la 5.

4. "Afadhali hivyo ulivyofanya. Kumbe watoto hawa tuliowadharau walikuwa nyota ya jaha. Sasa kijiji kina mwanga."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Bainisha toni katika dondoo hili. (alama 2)
(c) Fafanua dhima ya vipengele viwili vya kimtindo vinavyobainika katika dondoo hili. (alama 4)
(d) Fafanua umuhimu wa mzungumzaji katika kuijenga tamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 10)

5. (a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo: (alama 8)

"Kazi hizi nazo ni kama safari ya ahera; mwisho wake hakuna mwenye habari nayo. Basi imekuwa mfano wa gurudumu kwenye gari la masafa marefu. Lenyewe hilo linasukumwa tu. Linaviringishwa bila kupenda; halina hiari wala muhitari. Kazi yake kumenyana na ardhi; si pa mvua, si pa jua. Haijalishi kama kuna miba au mawe. Kwake mwendo ni wajibu. Yaani hata likachomeka haliwezi kufumua moto. Ndivyo maisha yetu yalivyo. Tunaendeshwa kama tiara. Upepo unatupiga tukiwa hewani huku mshika kamba pale chini anaona raha kwa sisi kuyumbishwayumbishwa."

(b) Onyesha jinsi usaliti unavyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 12)

Sehemu D: Ushairi

Jibu swali la 6 au la 7.

6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Ningekutana na ukweli ningeusabahi
Ningeupa shikamoo na kuupiga pambaja
Tukajenga mwema mlahaka
Kabla kuutazama kwa makini na
Kuuliza maswali.

Hakika ningetaka unieleze wapi ulibaki
Uongo ukipiga hatua na kupata umaarufu
Ningetaka kujua kwa nini haupendi ushindani
Kwa nini unaingia mitini wakati mno unahitajika
Na labda kwa nini umezoea kimya cha kutisha.

Natafuta ukweli katika chaka la mambo
Japo nasikia vazi lake linavaliwa na uongo
Nao wenyewe huo ukweli unakwenda tupu
Na watu tayari waukimbia kwa kuogopa
Kuona uchi wake.

Zimeshuka habari kutoka kwa kichaa mkongwe
Kuwa uongo amevaa suti ya ukweli
Ambayo aliiba wakiwa wanakoga mtoni
Na sasa watu wanaogopa kuuona uchi
Kama moto katika kichaka kikavu.

Wanaukimbilia uongo kuishangilia suti yake ambayo
Wanafahamu kuwa kaiba kwa kakake
Nyuma wameacha wingu la moshi
Liwatoalo watu machozi njia mbilimbili
Na vumbi zito la jivu linalowatia upofu.

— T. Arege

(a) Chambua maudhui katika shairi hili. (alama 4)
(b) Eleza sifa nne za ukweli kwa mujibu wa shairi hili. (alama 4)
(c) Jadili umuhimu wa mbinu rejeshi katika shairi hili. (alama 3)
(d) Onyesha umuhimu wa mbinu zifuatazo katika shairi hili: (i) tashihisi; (ii) sitiari. (alama 4)
(e) Bainisha uhuru wa kishairi katika shairi hili. (alama 3)
(f) Bainisha mifano ya matumizi ya chuku katika ubeti wa mwisho. (alama 2)

7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Binadamu ana kero, li ndani ya moyo wake,
Hupenda yalo mororo, yote yasadifu kwake,
Yanoleta mataguro, hukwepa yasimfike,
Hiyo ni yake kasoro, kiumbe binaadamu.

Milele katu hakiri, kupokonywa kilo chake,
Lakini huwa tayari, kudhulumu vya wenzake,
Na kujifanya hodari, kila lake liongoke,
Na hiyo yake kasoro, kiumbe binaadamu.

Kutwaa asichopewa, pia ni tabia yake,
Ubishi kabarikiwa, hivyo ni vilima vyake,
Kama hayo kitendewa, hakiri ikubalike,
Pia ni kasoro yake, kiumbe binaadamu.

Mwepesi wa kuchokoza, pia ni mtindo wake,
Ambae hajamuanza, humtafutia lake,
Na puresha kumjaza, mradi akasirike,
Nayo ni kasoro yake, kiumbe binaadamu.

Hakika binaadamu, kwa ule uzito wake,
Kawekewa jahanamu, likawe ni pigo lake,
Hiyo siku ya hukumu, adhabu zikamfike,
Kwa zile kasoro zake, kiumbe binaadamu.

(a) Kwa hoja sita, fafanua mtazamo wa mtunzi wa shairi hili kuhusu binadamu. (alama 6)
(b) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
(c) Bainisha vipengele vitatu vya kimtindo katika shairi hili. (alama 3)
(d) Fafanua aina tatu za uhuru wa kishairi katika shairi hili. (alama 3)
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)

Sehemu E: Fasihi Simulizi

8. (a) Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

(Ndani ya matatu. Mazungumzo yanazuka baada ya askari kuisimamisha.)

Askari: Habari dereva. Naomba kuona leseni yako.
Utingo: (Akijisemea.) Ni kubaya.
Dereva: (Akimnong'onezea Utingo.) Usiogope utachoma.
Askari: (Kwa dereva.) Mbona umeweka pesa ndani ya leseni yako?
Dereva: (Kwa sauti ya chini.) Tuliza boli afande! Ni kuchanganyikiwa tu.
Askari: Wewe dereva unaishi nyakati za kale! Hizi ni nyakati za kukomesha ufisadi. Kutoa chai barabarani ni msamiati wa mababu zetu.
Dereva: Sawa afande. Nimekuelewa vizuri.

 (i) Tambua utanzu wa Fasihi Simulizi unaowakilishwa na maneno yaliyokolezwa rangi katika mazungumzo haya. (alama 1)
 (ii) Bainisha sifa sita za utanzu uliotambua katika swali la (i). (alama 6)
(b) Unakusudia kutumia kinasa sauti kukusanya habari kuhusu tungo za aina hii.
 (i) Eleza manufaa saba ya kutumia mbinu hii. (alama 7)
 (ii) Fafanua changamoto sita za kutumia mbinu hii. (alama 6)

Marking scheme

Loading…

More Kiswahili papers