102/1 · KISWAHILI · Karatasi 1 (Insha) · Nov. 2023 · 1¾ saa
Maagizo: Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima. Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobaki. Kila insha isipungue maneno 400. Kila insha ina alama 20.
1. (Lazima) Wewe ni mtaalamu wa masuala ya kiuchumi katika Kaunti ndogo ya Inuka. Umegundua kuwa vijana wengi wanalalamika kuhusu uhaba wa nafasi za kazi. Andika barua kwa mhariri wa Gazeti la Mvule ukipendekeza njia mwafaka ambazo vijana wanaweza kutumia kujiimarisha kiuchumi. (alama 20)
2. Umetambua kwamba baadhi ya wanafunzi shuleni mwenu wanapuuza maadili yanayofaa kuzingatiwa wakati wa kula. Andika insha kuwaelimisha kuhusu maadili wanayopaswa kuzingatia wanapokula. (alama 20)
3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo: Kidole kimoja hakivunji chawa. (alama 20)
4. Tunga kisa kitakachomalizika kwa maneno yafuatayo:
… kila ninapokumbuka kisa hicho, ninapata matumaini kwamba maisha yangu yanaweza kubadilika. (alama 20)