102/1 · KISWAHILI · Karatasi ya 1 · INSHA · Machi 2022 (KCSE 2021) · Muda: Saa 1¾
Maagizo: Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima. Kisha chagua insha nyingine moja kutoka zile tatu zilizobakia. Kila insha isipungue maneno 400. Kila insha ina alama 20.
1. Lazima
Rafiki yako anasomea ng'ambo. Alipoondoka nchini, Kaunti yenu ilikuwa inakabiliwa na kutojitosheleza kwa chakula. Mwandikie barua kumweleza hatua ambazo Kaunti yenu imechukua kutatua tatizo hili.
2. Fafanua manufaa ya kuboresha miundomsingi nchini.
3. Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo: Aliye kando haangukiwi na mti.
4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:
"Maskini, anaonekana kuemewa na hisia za kupoteza. Huu mchezo wa bahati nasibu utakuja kutuangamizia kizazi," akajisemea Kutu huku akimtazama mja aliyekuwa kainamia meza huku ameshika kichwa…